Matokeo La Liga, Messi arudi na ushindi Suarez aendelea kucheka na nyavu

0
160

Bao la dakika ya 90 kutoka kwa nyota wa zamani wa
Fc Barcelona, Luis Suarez limeipa alama tatu muhimu
Atletico Madrid mbele ya Deportivo Alaves na kurejea
kileleni kwenye msimamo wa la liga.

Marcos Llorente aliifungia Atletico bao la kuongoza kabla
ya mlinzi Felipe kujifunga na kuisawazishia Alaves na wengi
Wakiamini mchezo umemalizika kwa sare ndipo Suarez akaweka
kambani bao la pili na la ushindi wa vijana wa Diego Simeone.

Lionel Messi amerejea dimbani na kutoa mchango
Mkubwa kwenye ushindi wa bao moja kwa bila waliopata fc
Barcelona dhidi ya Huesca bao pekee la Barca likifungwa na
Frank de Jong katika dakika ya 27.

Ushindi huo unawafanya Barca kupanda kwa nafasi moja hadi
katika nafasi ya tano wakifikisha alama 28 na kuishusha Sevilla
katika nafasi ya sita wakiwa na alama 26.

Matokeo ya mechi nyengine Atheltic Bilbao wamechomoza na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Elche wakati Granada wakitandikwa mabao mawili kwa bila na Eibar huku real Sociedad na Osasuna wakitoka sare ya bao moja kwa moja.