Mashindano ya Olimpiki 2020 kufungwa leo

0
597

Mashindano ya Olimpiki mwaka 2020 yanatazamiwa kufungwa rasmi leo mjini Tokyo, Japan ambapo taifa la Tanzania liliwalikishwa na wanariadha watatu.

Mashindano hayo yalipaswa kufanyika mwaka jana katika majira ya joto lakini yaliahirishwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO-19, hivyo yakaanza Julai 23, 2021 mpaka leo Agosti 8, 2021.

Katika mashindano hayo Tanzania iliwakilishwa na wanariadha Failuna Matanga, Gabriel Geay na Alphonce Simbu ambaye usiku wa kuamkia leo alifanikiwa kukimbia mbio ndefu za kilomita 42.2 na kushika nafasi ya 7 akiwa ameshuka nafasi mbili ikilinganishwa na mara ya mwisho alipokimbia mbio hizo ambapo alishika nafasi ya tano.

Katika mbio hizo ambazo zilishirikisha wakimbiaji 106 zikiwakilisha nchi 45 , Eliud Kipchoge kutoka nchi Kenya alishinda mbio. Kipchoge anakuwa mkimbiaji wa tatu katika historia kushinda mbio hizo mfululizo akiungana na wakimbiaji wengine Abele Bikila (1960,1964) na Waldemar Cierpinski (1976,1980).

Taifa la Kenya ndio taifa lililofanya vizuri zaidi Kati ya mataifa ya Afrika ambapo hadi leo tayari limejikusanyia medali 10, huku Tanzania ikiwa haina medali.