Arsenal imeendelea kuonesha kuwa inalitaka taji la Ligi Kuu ya England msimu huu ambapo imeendelea kutoa kipigo kwa kila timu inayokutana nayo, tena kwa idadi kubwa ya magoli.
Katika mchezo wake wa mwisho iliyocheza dhidi ya Sheffield United imeibuka na ushindi wa magoli 6-0 na kufikisha jumla ya magoli 24 katika michezo yake mitano kwenye EPL.
Mchuano wa taji hilo unazidi kuwa mkali ambapo Liverpool inaongoza ligi ikiwa na alama 63, ikifuatiwa na Manchester City na Arsenal zenye alama 62 na 61, mtawalia.
Unaiona Arsenal ikifanikiwa kubeba ubingwa wake wa kwanza wa EPL baada ya miaka 21?