Maradona na goli la mkono wa Mungu

0
154

Diego Armando Maradona, Dunia inamchukulia kama moja ya wachezaji bora wa kandanda kuwahi kutokea kwenye sayari hii yenye makazi ya watu toka kwenye mabara saba.

Mchezo wa kukumbukwa zaidi na umekuwa kuwa historia inayokumbwa zaidi kwa Diego Maradona ni ule wa robo fainali dhidi ya England ambapo Maradona alifunga magoli kwenye ushindi wa bao mbili kwa moja huku goli la kwanza akifunga kwa mkono na goli hilo kubatizwa jina la ‘HAND OF GOD’ na goli la pili alionyesha maajabu kwa kuwalamba chenga wachezaji wa England pamoja na kipa wao Peter Shilton.

Goli ambalo hadi leo linachukuliwa kuwa ndio goli bora zaidi kwenye michuano ya kombe la Dunia na magoli yote hayo mawili aliyafunga ndani ya dakika tatu tu.

Jezi yake Diego Maradona aliyoivaa kwenye mchezo aliofunga goli kwa mkono ilipigwa mnada kwa bei ya Dolla Million 9.3 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 18 za Kitanzania na jezi hiyo alikuwa nayo mchezaji wa England  Steve Hodge ambae alibadilishana na Maradona jezi hiyo mara baada ya mchezo huo kumalizika mwaka 1986.

Na Mpira aliotumia kufunga goli hilo la Mkono wa Mungu unapigwa mnada na muamuzi aliechezesha mchezo huo anaeitwa Ali Bin Nasser toka Tunisia na bei yake ni Dolla Milioni tatu ambazo ni zaidi ya Bilioni sita na Milioni mia Tisa za Tanzania.

Nguli huyo alifariki dunia Novemba 25/2020 kwa mshtuko wa moyo na kuzikwa kwenye makaburi ya  Bella Vista huko kwenye mji mkuu wa Argentina wa Buenos Aires na kutamatisha maisha yeka hapa duniani alikoishi kwa miaka 60 na siku 26 ila ndie mtu anaheshimika mno kwenye kandanda nchini Argentina na Duniani kwa ujumla.

Bado siku 11, kaa tayari kutazama na kusikiliza Fainali za Kombe la Dunia kupitia TBC buuree kuanzia Novemba 20 – Disemba 18.