Mapokezi makubwa kwa Tunisia Qatar

0
184

Timu ya Taifa ya Tunisia imepata mapokezi makubwa ilipowasili katika mji mkuu wa Qatar, Doha tayari kwa michuano ya Kombe la FIFA la Dunia inayotarajiwa kurindima kuanzia Jumapili wiki hii.

Tunisia ambayo imepangwa kundi D pamoja na mabingwa watetezi Ufaransa, Australia na Denmark imewasili usiku wa kuamkia leo nchini humo.

Watunisia wengi wanaoishi Mashariki ya Kati pamoja na mashabiki waliosafiri, wamejitokeza kuilaki timu yao ya Taifa huku wakiwa na matumani ya kufanya vema.

Tunisia ni miongoni mwa Mataifa matano ya Afrika yanayowakilisha Bara hilo kwenye michuano ya Kombe la FIFA la Dunia mwaka huu.

Nchi nyingine ni Ghana, Morocco, Cameroon na Senegal.