Mane na Cancelo kuondoka Bayern Munich

0
410

Sadio Mane na Joao Cancelo wanatarajiwa kuondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu, Sky Germany imeeleza.

Bayern ina kipengele cha kumnunua Cancelo aliyetokea Manchester City kwa mkopo, lakini imeweka wazi kuwa haiko tayari kulipa TZS bilioni 176 zaidi kumsaini nyota huyo wa Ureno.

Mane ambaye amekuwa na msimu mmoja ndani ya miamba hiyo ya Ujerumani akitokea Liverpool FC atawekwa sokoni.

Katika msimu huu, Mane ambaye alikumbwa na majeraha amefunga magoli 12.