Mane Mchezaji Bora Afrika 2019

0
480

Mshambuliaji Sadio Mane (Senegal) anaekipiga na Mabingwa wa dunia klabu ya Liverpool ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika akiwashinda wachezaji wenzake Mohamed Salah wa Misri na Riyard Mahrez wa Algeria

Kwa upande wake Riyad Mahrez ameshinda Tuzo ya goli bora la mwaka 2019 huku timu yake ya Algeria ikichaguliwa kuwa timu Bora Afrika kwa Mwaka 2019

Katika Tuzo hizo zinazotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zilizofanyika Nchini Misri katika fukwe za Hurghada Msanii pekee kutoka Tanzania alipata fursa ya kutumbuiza katika hafla hiyo huku akiwanyanyua wachezaji nguli na viongozi wa soka Duniani kwa vibao vyake alivyoimba katika usiku wa Tuzo hizo