Mane aachwa kwa madai wa kumpiga Leroy Sane

0
712

Bayern Munich wamemwacha Sadio Mane nje ya kikosi chao kitakachocheza mchezo wa ligi Jumamosi dhidi ya Hoffenham, huku kukiwa na madai kuwa alimpiga mchezaji mwenzake Leroy Sane.

Ripoti kutoka Ujerumani zinadai Mane alimgonga Sane usoni kufuatia kichapo cha 3-0 kwenye Ligi ya Mabingwa kutoka kwa Manchester City, hatua iliyopelekea kuamuliwa na wachezaji wenzao.

Bayern imesema mshambuliaji huyo wa Senegal ameachwa kwa sababu ya “utovu wa nidhamu” na kuthibitisha kuwa pia atapigwa faini.

Mane, ambaye ni Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika mara mbili, alilalamika kuhusu jinsi winga wa Ujerumani Sane alivyozungumza naye baada ya kushindwa.

Baada ya kurejea Ujerumani Mane aliondoka na usafiri binafsi huku Sane akiondoka na basi la timu. Hadi sasa hakuna kati yao aliyezungumzia hilo.

Jumatano Bayern wataikaribisha Manchester City kwenye mchezo wa marudiano wakiwa na mlima mkubwa wa kupanda.