Manchester City Mabingwa Ulaya 2022/2023

0
214

Manchester City imetwaa taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Inter Milan ya Italia usiku wa jana uwanja wa Atatürk Olimpiyat jijini İstanbul nchini Uturuki.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa Kimataifa wa Hispania, Rodrigo Hernández Cascante ‘Rodri’ dakika ya 68 na hilo linakuwa taji la tatu la msimu kwa kocha Mspaniola, Pep Guardiola baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England na Kombe la FA.