Manchester United na Chelsea jana zimerejea kwenye Ligi Kuu ya England (EPL) kwa ushindi katika michezo yao ya mzunguko wa 15 wa ligi hiyo.
Chelsea waliwanyuka FC Bournemouth mabao 2 kwa bila katika mchezo wa mapema uliopigwa katika dimba la Stanford Bridge jijini London.
Mabao ya Chelsea yaliyofungwa na nyota wa Ujerumani, Kai Havertz dakika ya 16 na Mason Mount dakika ya 22 yametosha kuipa alama tatu klabu hiyo inayoshika nafasi ya 8 ya msimamo wa EPL.
Mchezo wa baadaye ukawashuhudia mashetani wekundu, Manchester United wakiibamiza Nottingham Forest mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Old Trafford mjini Manchester.
Mabao ya United yamefungwa na Marcus Rashford, Anthony Martial na Fred.