Manchester City wameshtakiwa kwa zaidi ya makosa 100 ya ukiukaji mkubwa wa sheria za kifedha za Ligi Kuu ya England (EPL) kufuatia uchunguzi wa miaka minne kuhusu dili zao.
NINI KIMETOKEA? Klabu hiyo ambayo imetwaa mataji manne ya EPL katika misimu mitano iliyopita wamebainika kuwa na matumizi makubwa ya pesa yakiruhusu timu ya Pep Guardiola kuendelea kuwa na ushindani katika nyanja nyingi.
Mmiliki wa klabu hiyo, Sheikh Mansour ameendelea kutoa mabilioni ya fedha ndani na nje ya uwanja katika miaka 14 ya uongozi wake.
Shirikisho la Soka nchini England limekuwa likifuatilia matumizi yao ya fedha na sasa limeamua hatua zichukuliwe baada ya kubaini ukiukwaji mkubwa wa sheria.
NINI KITATOKEA? City sasa wanangoja kujua ni hatua gani itachukuliwa dhidi yao, wakati ikiendelea kuwania ubingwa wa EPL, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa msimu wa 2022-23.
Hata hivyo, wataalamu wa fedha za soka wameeleza kuwa hakuna adhabu inayoweza kuondolewa katika hatua hii ya awali.