Man City yaitupa nje Arsenal FA Cup

0
288

Manchester City imewatupa Arsenal nje ya michuano ya Kombe la FA ambao ni washindani wao katika Ligi Kuu ya England (EPL).

Goli pekee la dakika ya 64 la beki Nathan Ake lilitosha kuipa City ushindi ikikutana na Arsenal kwa mara ya kwanza katika msimu huu ambapo kwenye EPL bado hazijakutana.

Ushindi huo unaiweka City katika nafasi nzuri ya Kisaikolojia pindi itakapokutana tena na vinara hao wa EPL katikati ya Februari mwaka huu kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa ligi.

Guardiola ameendeleeza ubabe dhidi ya Arteta ambaye alikuwa msaidizi wake, katika kile kinachoonekana kuwa mwanafunzi hawezi kushinda mwalimu.