Man City mabingwa EPL mara ya 4 mfululizo

0
352

Klabu ya Manchester City imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa English Premier League (EPL) baada ya kuifunga klabu ya West Ham United magoli 3-1 na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kubeba taji hilo mara nne mfululizo.

City inachukua ubingwa baada ya kufikisha pointi 91, ikifuatiwa na Arsenal yenye alama 89 baada ya kushinda magoli 2-1 dhidi ya Everton katika michezo ya kukamilisha msimu wa 2023/24

Erling Halland ameibuka kuwa mfungaji bora wa msimu kwa kufikisha magoli 27

Wape neno moja la kuwafariji mashabiki wa Arsenal!