Man City bingwa Carabao

0
991

Timu ya Manchester City imetwaa kikombe cha  Carabao baada ya kuitandika Chelsea kwa mikwaju ya penati minne kwa mitatu  katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Wembley .

Ndani ya dakika 120,  timu hizo hazikuweza kufungana ndipo mikwaju ya penati ikapigwa.

Katika muda wa nyongeza, kocha wa Chelsea alifanya mabadiliko ya golikipa,  lakini golikipa Kepa Arrizabalaga aligoma kutolewa jambo lililofanya Kocha Maurizio Sarri kushikwa na hasira.

Mchezaji Leroy Sane ndiye alikosa penati kwa upande wa Manchester City,  huku mchezaji wa kwanza kupiga penati kwa upande wa Chelsea,- Jorge Luiz Frello Filho (Jorginho) shuti lake likiokolewa na golikipa wa Man City  na mchezaji  David Luiz  shuti lake likagonga mwamba .