Ligi Kuu England imeendelea leo kwa michezo miwili, mechi ya kwanza Southampton imepokea kipigo cha mabao 2 kwa 1 dhidi ya Burnley
Mechi ya pili Liverpool wakiwa ugenini katika dimba la Carrow road wameibuka na ushindi mwembamba wa bao moja kwa bila dhidi ya Norwich city bao pekee likifungwa na Sadio Mane dakika ya 78
Hapo kesho Aston Villa wakitumia uwanja wao wa Villa Park watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Tottenham Hotspur wakati Arsenal wakichuana vikali dhidi ya Newcastle United