Liverpool yapaa kileleni

0
179

Majogoo ya jiji Liverpool wameibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa ligi kuu England uliopigwa katika dimba la Anfied na kushika usukani wa ligi hiyo

Liverpool walianza kwa kasi mchezo huo na kupata bao la kuongoza dakika ya 26 kupitia kwa Mohamed Salah, dakika ya 33 Tottenham wanarudi mchezoni baada ya Hueng-min Son kufunga bao la kusawazisha

Bao la lala salama kutoka kwa Roberto Firmino dakika ya 90 linaipa ushindi na alama 3 muhimu Liverpool na kufikisha jumla ya alama 28 baada ya michezo 13 wakiwa mbele ya Tottenham inayoshika nafasi ya 2 wakibaki na alama zao 25