Liverpool yachezea kipigo dhidi ya Wolves

0
393

Liverpool imechezea kichapo cha magoli matatu kutoka kwa mbwa mwitu, Wolves, ikiwa ni mwendelezo mbaya wa vijana wa Jurgen Klopp.

Goli la kujifunga la Joel Matip, goli la mchezo wa kwanza Craig Dawson na goli la Ruben Neves yalitosha kulinyamazisha jiji la Liverpool.

Liverpool wamepoteza mchezo wa tatu mfululizo ugenini, ikiwa ni mwenendo mbaya wa klabu hiyo ambayo ipo katika nafasi ya 10.

Wakati hali ikiendelea kuwa mbaya kwenye Ligi Kuu ya England, ambapo hawapo kwenye nafasi ya kuwania ubingwa, kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya watacheza dhidi ya Real Madrid Februari 21 na Machi 15, 2023.