Majogoo ya Jiji Liverpool wamezidi kujiimarisha kileleni mwa ligi kuu ya England baada ya kuitandika Manchester United mabao 2 kwa nunge katika mchezo huo wa ligi uliopigwa dimba la Liverpool, Anfield
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Van Dijk dakika ya 14 na bao la pili likifungwa dakika ya 90 ya mchezo huo na mshambuliaji hatari Mohamed Salah baada ya Liverpool kucheza (counterattack) dhidi ya Manchester United na kufanikiwa kunyakuwa alama 3 muhimu
Katika mchezo wa awali Leicester City imekubali kichapo cha mabao 2 kwa 1 dhidi ya Burnley na kuendelea kubaki katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi.