Liverpool Vs Real Madrid hatua ya 16 bora

0
155

Droo ya hatua ya 16 bora ya ligi ya Mabingwa Barani Ulaya imefanyika hii leo ambapo mabingwa mara 6 wa ligi hiyo Liverpool wataanzia nyumbani dhidi ya mabingwa mara 14 wa michuano hiyo Real Madrid.

Mchezo mwingine utakaovuta hisia za wapenzi wa kandanda ulimwenguni ni ule utakaowakutanisa mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich na mabingwa wa Ufaransa PSG, ambao mkondo wa kwanza unatarajiwa kufanyika mjini Paris.

Mabingwa mara mbili wa ligi hiyo Chelsea watakua ugenini kutifuana na Borussia Dortmund katika mchezo mwingine ambao unatajwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mabingwa wa Italia AC Milan wataanza nyumbani kwa kuwaalika Tottenham Hotspurs huku ndugu zao wa Inter Millan wakiwa wenyeji wa FC Porto ya Ureno.

Michezo mingine katika hatua hiyo ambayo ni ya mtoano ni kati ya mabingwa wa England Manchester City dhidi ya RB Leipzig ya Ujerumani, Club Brugge wakiwa wenyeji wa miamba ya Ureno Benfica na mchezo wa mwisho utakuwa baina ya Frankfurt ya Ujerumani dhidi ya Napoli ya Italia.

Mkondo wa kwanza wa mzunguko huo utachezwa Februari 14-15, 2023 na Februari 21-22, 2023.

Marudio ya michezo hiyo yatafanyika Machi 7-8 na Machi 14-15, 2023