Liverpool dhidi ya Real Madrid fainali Uefa

0
322

Majogoo ya Jiji, Liverpool waliotangulia mapema katika fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kuitandika Villareal kwa jumla ya mabao 5 kwa 2 katika michezo miwili iliyopigwa nyumbani na ugenini watacheza na miamba ya soka kutoka Hispania, Real Madrid

Madrid imesonga mbele kibabe baada ya kuitandika Manchester City kwa jumla ya mabao 6 kwa 5 katika michezo miwili waliyocheza nyumbani na ugenini huku mchezo wa mwisho uliopigwa usiku wa jana ukidhihirisha uzoefu na ukubwa wa timu hiyo katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya

Mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya 2021/2022 utapigwa May 28 katika Dimba la Mtakatifu Denis mjini Paris, Ufaransa.