Ligi Kuu ya England imesimamishwa hadi Aprili 3 mwaka huu kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, wakati ambapo baadhi ya wachezaji wametengwa katika maeneo maalum baada ya kuonesha dalili za virusi hivyo.
Mashindano mengine nchini humo ambayo ni pamoja na ligi ya mabingwa, ligi ya EUROPA, kombe la shirikisho yamesimamishwa kwa muda kutokana na baaadhi ya wachezaji kuathirika, huku Arsenal ikifunga uwanja wa mazoezi kutokana na kocha Mikel Arteta kuugua COVID-19.
Shirikisho la Soka nchini England limesema kuwa michezo itarejea tena Aprili 4, lakini kwa kuzingatia ushauri wa kitabibu.
Uamuzi huo umekuja wakati mchezaji wa Chelsea Hudson-Odoi ameathirika huku Everton ikiripoti kuwa mmoja wa wachezaji wake pia ameathirika.