Lampard akalia kuti kavu

0
176

Kipigo cha mabao matatu kwa moja walichopata
Chelsea kutoka kwa Manchester city wakiwa nyumbani pale
Stamford Bridge kinazidi kumuweka katika shinikizo kubwa
meneja wa kikosi hicho Frank Lampard

Wakiwa katika ubora wa hali ya juu vijana wa man city walionesha kuwa Lampard hatoshi kuwanoa the blues kwa kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo na kujipatia mabao matatu yaliyowekwa wavuni na Ilkay Gundogan, Phil Foden na Kevin de Bruyne


Ushindi huo unawafanya Man city kuchupa hadi katika nafasi ya 5
kwenye msimamo wa ligi kuu ya England wakifikisha alama 29
walizovuna katika michezo 15 wakati chelsea wao wanaporomoka
hadi katika nafsi ya 8 wakiwa na alama zao 26 wakiwa wameshuka
dimbani katika michezo 17.

Kwingineko Leicester city wameishusha Tottenham
Hotspur na kupanda hadi katika nafasi ya tatu wakifikisha alama
32 baada ya kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya
Newcastle united na mchezo kati ya Burnley dhidi ya Fulham ukiahirishwa kutokana na idadi kubwa ya wachezaji wa Fulham kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.


Hii leo vinara wa ligi hiyo majogoo wa jiji Liverpool wenye alama
32 watakuwa ugenini kwenye dimba la st. Marry’s kusaka alama
tatu muhimu mbele ya Southampton waliopo katika nafasi ya
tisa wakiwa na alama 26.