Kocha wa SIMBA apigwa ‘spana’

0
268

Klabu ya Simba imevunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi hicho Zoran Maki.

Taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez imesema, Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili na pia wamesitisha mkataba na kocha wa viungo Sbai Karim pamoja na Kocha wa Makipa Mohammed Rachid.

Kwa sasa timu hiyo ipo chini ya Kocha Msaidizi Selemani Matola na tayari mchakato wa kumtafuta kocha mpya umeanza.