Kocha wa Ruvu Shooting FC atozwa faini na kufungiwa

0
387

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemtoza faini ya shilingi milioni 1 Kocha Msaidizi wa Ruvu Shooting FC, Renatus Shija kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano na mtangazaji Azam TV, televisheni ya mdhamini mwenye haki ya matangazo ya televisheni.

Shija alikataa kufanya mahojiano hayo baada ya mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons FC ambapo Wazee wa Mpapaso (Ruvu Shooting) walipoteza kwa magoli 3-1.

Aidha, kocha huyo amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya shilingi milioni 1 kwa kosa la kuwatolea lugha ya matusi wafanyakazi wa Azam TV waliokuwa wakimsihi akubali kufanya mahojiano.

Ruvu Shooting ipo katika hatari ya kushuka daraja ambapo ipo nafasi ya pili kutoka mwishoni ikiwa na alama 20 baada ya kushuka dimbani mara 26.