Mchezaji wa mpira wa kikapu wa zamani wa Marekani Kobe Bryant amefariki katika ajali ya Helicopter California Marekani baada ya chombo hicho kushika moto.
Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa watu 5 waliokuwa wakisafiri safari binafsi wamefariki kwenye ajali hiyo ya Helicopter akiwemo Kobe Bryant.
Bryant amefariki akiwa na umri wa miaka 41 alizaliwa Agosti 23, 1978.
Bryant alicheza mpira wa kikapu kwa miaka 20 na Los Angeles Lakers na kutwaa Ubingwa wa Chama cha Taifa cha Mpira wa Kikapu (NBA) na kustaafu mchezo huo April 2016.