Klabu za EPL zarejea rasmi mazoezini

0
1011

Klabu zinazoshiriki ligi kuu ya kandanda ya England zimekubaliana kuanza mazoezi kwa makundi  ya wachezaji wachache kuanzia hii leo.

Masharti yaliyotolewa na mamlaka zinazosimamia afya nchini humo ni pamoja na wachezaji kuzingatia utaratibu wa kuachiana nafasi na kutoshikana kwa namna yoyote wawapo mazoezini.

Taarifa ya Chama cha soka cha England (FA) imezitaka klabu zote zinazoshiriki ligi kuu kuhakikisha zinatoa kipaumbele kwenye suala la afya za wachezaji na kuweka mazingira yanayofaa kwa wachezaji kufanya mazoezi.

Taarifa hiyo ya FA imetaka kuwe na utayari kwa wachezaji kurejea mazoezini katika makundi hayo  ya wachezaji wachache na baadae wachezaji wote watajumuika pamoja.