Kitayosce na Fountain Gate zafungiwa kusajili

0
303

Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limezifungia klabu za Kitayosce na Fountain Gate za Tanzania kufanya usajili wa wachezaji kimataifa.

Rungu hilo la FIFA limezishukia klabu hizo baada ya kocha Ahmed El Faramawy Yosef Mostafa Soliman kushinda kesi za madai dhidi ya vilabu hivyo ambapo alipinga kuvunjia mikataba kinyume cha taratibu.

Baada ya Soliman kushinda vilabu hivyo vilitakiwa viwe vimemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi ulipotolewa, jambo ambalo halijafanyika.

Wakati klabu hizo zikikabiliwa na adhabu hiyo ya FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezifungia kufanya uhamisho wa wachezaji ndani ya nchi.

Kitayosce inashiriki Ligi Kuu ya NBC na Fountain Gate inashiriki Ligi ya Championship.