Kim Poulsen Kocha mpya Taifa Stars

0
168

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Kim Poulsen, raia wa Denmark, kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kim ambaye aliwahi pia kuwa kocha wa timu hiyo mwaka 2012 na 2013, anachukua nafasi ya Mrundi Etienne Ndayiragije ambaye mkataba wake wa kuinoa Stars ulisitishwa baada ya kumalizika mashindano ya CHAN na Tanzania kuondolewa katika hatua ya makundi.

Taarifa ya TFF imesema kuwa tayari Kim amesaini kandarasi ya kuinoa timu hiyo ambayo inajiandaa na michuano ya kufuzu kwa AFCON mwaka 2022 nchini Cameroon na michuano ya kufuzu kwa kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.