Karia ajitosa tena Urais TFF

0
221

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amechukua fomu ya kuwania Uraisi wa shirikisho hilo katika zoezi lililoanza hii leo.

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Swedy Nkwabi ndiye aliyechukua fomu kwa niaba ya Karia.

Wengine waliochukua fomu hii leo kuwania nafasi hiyo ya Urais wa TFF katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti 7 mwaka huu ni Evans Mgeusa na Zahor Mohammed Haji.