Kagera Sugar vs Yanga CCM Kirumba

0
212

Klabu ya soka ya Yanga hii leo inashuka katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza kuwakabili wana nkurukumbi Kagera Sugar katika muendelezo wa Michezo ya Ligi Kuu ya soka ya NBC.

Mchezo huo ambao pia ni muhimu kwa Kagera Sugar ambayo inajikusanya kurejea makali yake unatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Yanga itamkosa nyota wake Stephen Aziz Ki ambaye amefungiwa michezo mitatu na Djuma Shaban ambaye ni majeruhi.

Mchezo mwingine wa ligi hiyo utapigwa katika dimba la Sokoine jijini Mbeya ambapo Mbeya City watakuwa wenyeji wa Coastal Unioni ya Tanga.

Mchezo baina ya timu hizo utakua mkali na kutokana na vikosi vya timu zote mbili lakini pia kila timu ikisaka alama tatu muhimu hii leo. kuu ya soka ya NBC.

Yanga iliyotokea Tunisia ambapo ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika inazisaka alama tatu ili irejee kileleni mwa Ligi hiyo.