Bodi ya ligi kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kuahirisha mechi ya ligi kati ya wenyeji Kagera Sugar dhidi ya Wekundu wa Msimbazi Simba ambao ulikuwa upigwe leo saa kumi alasiri katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
Mchezo huo namba 69 wa ligi kuu NBC umeahirishwa kutokana na taarifa za kitabibu kuwa wachezaji 16 kati ya wachezaji 22 wa Simba sc waliosafiri kwenda Bukoba kwenye mchezo huo kuonekana kuwa na dalili za mafua na kukohoa hali inayochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa
Kwa mujibu wa kanuni ya 34:1(1.3) ya ligi kuu , mchezo huo umehairishwa na utapangiwa tarehe nyengine ikiwa ni kwa mujibu wa kanuni ya 34:2 ya ligi kuu