Jonas Mkude Atozwa faini, atakiwa kurejea kambini

0
225

Kamati ya nidhamu ya klabu ya Simba chini ya mwenyeki wake Suleiman Kova imetangaza hukumu ya kiungo wa klabu hiyo, Jonas Mkude ambaye alisimamishwa na uongozi kwa makossa ya utovu wa nidhamu.

Kwa mujibu a Kova, amesema Mkude ametozwa faini ya shilingi milioni 2 kutokana na makosa matatu ambayo ni kutohudhuria semina elekezi iliyohusisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi.

Adhabu yake ni faini ya shilingi milioni moja (1,000,000).

Pia kuchelewa kuingia kambini wakati timu ilipokuwa ikijiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union. Adhabu aliyopewa ni karipio kali na faini ya shilingi milioni moja (1,000,000) na kuwekwa katika kipindi cha uangaizi cha miezi sita.

Na kutoripoti kambini siku ya 26/11/2020 bila ruhusa. Katika tuhuma hizi, kamati haikumkuta na hatia baada ya kamati kutothibitisha pasipo shaka shitaka hilo.

Kamati imemtaka Mkude kurejea kambini mara moja kuendelea na mazoezi na asipofanya hivyo atakuwa amefanya tena kosa la utovu wa nidhamu.

Faini aliyotozwa anatakiwa kuilipa ndanI ya mwezi mmoja.

Kamati imemtaka Mkude kuomba radhi kwa maandishi ndani ya saa 24