JKT Queens mabingwa Ligi ya Wanawake

0
486

JKT Queens ndio bingwa wa Ligi ya Wanawake Tanzania Bara kwa msimu wa 2022/23 ikiwa na alama 46 katika michezo 18.

Mabingwa hao wamemaliza msimu bila kupoteza mchezo hata mmoja wakiwa wameshinda michezo 14 na kwenda sare minne.

Simba Queens imeshika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikienda kwa Fountain Gate Princess huku The Tihers Queens na Mkwawa Queens zikishuka daraja.

Huu ni ubingwa wa tatu kwa JKT Queens ambapo wamechukua kombe hilo kutoka kwa Simba Queens ambao walitwaa kombe hilo mara tatu mfululizo.