JKT Queens kuiwakilisha Tanzania nchini Uganda

0
297

JKT Queens inatarajia kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Baraza la Mashirikisho ya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yatakofanyika nchini Uganda kuanzia Agosti 12 hadi 30 mwaka huu.

JKT Queens inaendelea na maandalizi mkoani Kagera, eneo ambalo linawapa wachezaji urahisi wa kuzoea mazingira na hali ya hewa ya Uganda kwani mkoa wa huo upo karibu na nchi hiyo.

Timu hiyo ipo Kundi B na timu za Kihija kutoka Kenya, New Generation kutoka Zanzibar na AC Kigali kutoka Rwanda.

JKT Queens inashiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza baada ya kuwa bingwa wa Ligi ya wanawake Tanzania Bara msimu wa 2022/23.

Mashindano hayo ni fursa nzuri kwa JKT Queens kuonyesha uwezo wao, kuendeleza mchezo wa soka kwa wanawake, na kuwa na mchango katika kukuza mazingira bora ya michezo.