Ihefu sasa kuitwa Singida Black Stars SC

0
704

Timu ya soka ya Ihefu iliyohamisha makazi yake kutoka Mbarali, Mbeya na kwenda Singida, imebadili jina lake kutoka Ihefu Sports Club na sasa inatambulika kama Singida Black Stars Sports Club.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo imesema lengo la kubadili jina hilo ni kuiunganisha timu na wananchi wote wa Mkoa wa Singida.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Singida Black Stars Sports club (zamani Ihefu SC) imelenga katika kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana wa Kitanzania ili kuinua maisha yao na kutimiza ndoto zao kupitia vipaji walivyonavyo.