Ihefu kuendeleza ubabe dhidi ya Yanga?

0
465

Ihefu SC imekuwa mwiba kwa Yanga SC kwa msimu miwili ambapo msimu uliopita walitibua rekodi ya Yanga ya kutopoteza michezo 49 baada ya kuifunga 2-1 katika Uwanja wa Highland Estate, Mbeya, ambapo Yanga ilihitaji kushinda mchezo huo ili kufikisha michezo 50 bila kupoteza.

Kama hiyo haikutosha, Oktoba 2023 Ihefu ilitia doa safari ya ushindi ya Yanga baada ya kuifunga magoli 2-1, ikiwa ni kipigo cha kwanza kwa Yanga katika michezo nane iliyokuwa imecheza.

Leo timu hizi zinakutana tena katika dimba la Azam Complex, Dar es Salaam ambapo Yanga inaongoza ligi ikiwa na alama 46, huku Ihefu ikiwa nafasi ya nane ikiwa na alama 23. Katika michezo mitano ya mwisho ya ligi, Yanga imeshinda yote huku Ihefu ikishinda mitatu, sare moja na kupoteza mmoja.

Je, yaliyotokea katika mechi mbili za mwisho ambazo Ihefu ilishinda yatajirudia? Au Yanga itafuta uteja na kujiimarisha kileleni?

Usikose kusikiliza mchezo huu mbashara kupitia TBC Taifa na ukurasa wa YouTube wa TBCOnline kuanzia saa 11:30 jioni leo.