Hispania kuendelea kusimamisha ligi kwa muda usiojulikana

0
1444

Shirikisho la Soka nchini Hispania (RFEF) limetangaza kuendelea kuisimamisha Ligi Kuu ya nchi hiyo La Liga na mashindano mengine yote kwa muda usiojulikana.

RFEF imefikia uamuzi huo kufuatia kuongezeka kwa maambukizi ya homa ya corona, pamoja na vifo vinavyotokana na homa hiyo.

Katika taarifa yake, Shirikisho hilo la soka nchini Hispania limesema kuwa hawataendelea na msimu wa mashindano mpaka hapo serikali ya nchi hiyo itakapotoa tamko kuhusu virusi vya corona.