HAALAND AKERWA NA MWAMUZI

0
494

Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland amemkosoa vikali Simon Hooper kupitia mitandao ya kijamii kufuatia uamuzi wake wakati wa mchezo dhidi ya Tottenham uliomalizika kwa sare ya 3-3.

Haaland alikerwa na uamuzi wa mwamuzi kupuliza filimbi wakati ambao Jack Grealish alikuwa kwenye nafasi ya kufunga, kitendo ambacho raia huyo wa Norway alikitafsiri walinyimwa nafasi ya kufunga goli.

Mwamuzi aliwapa City ‘advantage’ ya kuendelea kucheza baada ya Haaland kuchezewa faulo, lakini baada ya kutoa pasi kwa Grealish aliyekuwa amebaki dhidi ya kipa, mwamuzi alisimamisha mchezo kutoka na faulu hiyo.