Rekodi ya Mshambuliaji wa Ufaransa, Antoine Griezmann ya kucheza michezo ya timu ya taifa mfululizo tangu Novemba 2016 imefikia ukingoni baada ya kuondolewa kwenye kikosi hicho kitakachocheza mechi za kirafiki dhidi ya Ujerumani na Chile.
Griezmann ambaye hadi kuondolewa kwake kikosi alikuwa amecheza michezo 84 mfululizo, ameondolewa kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu (ankle).
Les Bleus na mataifa mengine ya Ulaya yanajiandaa na michezo ya Euro 2024 ambayo inatarajiwa kutimu vumbi kuanzia Juni 14 hadi Julai 14 mwaka huu.