Mwanariadha wa Tanzania, Gabriel Geay ameiwakilisha vema Tanzania katika mbio za “2022 Athletics World Championships” zilizofanyika nchini Marekani, kwa kuingia 10 bora.
Geay mwenye umri wa miaka 26, amemaliza mbio hizo katika nafasi ya saba kwa kutumia muda wa saa 2:07:31 huku washindi namba moja hadi tatu wakitumia muda wa kati ya saa 2:05:36 na saa 2:06:48
Katika mashindano mbalimbali ya mbio ya kimataifa, Geay amekuwa akiiwakilisha Tanzania na kushika nafasi za juu zenye kuiweka nchi kwenye ramani ya mashindano hayo ya riadha.