Everton yaikanda Arsenal

0
310

Baada ya kwenda miezi mitatu bila kupata ushindi, Everton leo imeondoka na alama tatu baada ya kuifunga Arsenal, ukiwa ni mchezo wa kwanza wa kocha Sean Dyche.

Kwa kipigo hicho, Arsenal inakuwa imepoteza mchezo wa pili msimu huu, hivyo kuendelea kupunguza utofauti wa alama kati yake na Manchester City, ambapo kwa sasa zimepishana kwa alama 5.

Arsenal ipo kileleni mwa ligi ikiwa na alama 50 baada ya kucheza mechi 20, huku Everton ikiwa nafasi ya 17 na alama 18 baada ya mechi 21.