Europa yaendelea bila mashabiki

0
1277

Michuano ya Ligi ya Europa imeendelea kupigwa bila mashabiki katika miji tofauti barani Ulaya

Manchester United wakiibuka na ushindi mnono wa mabao 5 kwa bila dhidi ya LASK ya Austria

Mabao ya United yakifungwa na Odion Ighalo, Daniel James, Juan Mata, Greenwood na Andreas Pereira

Nao wababe wa Arsenal, timu ya Olympiacos ya Ugiriki wamelazimishwa sare ya kufungana bao moja kwa moja dhidi ya Wolves

Rangers wakiwa nyumbani wamenyukwa mabao 3 kwa 1 dhidi ya Bayer Leverkusen wakati Fc Basel wakiitandika Eintranch Frankfurt mabao matatu kwa bila na Wolfsburg wakitandikwa mabao mawili kwa moja na Shakhtar Donetsk