Droo ya mashindano makubwa Afrika Machi 12

0
916

Droo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2023/2024 na Kombe la Shirikisho Afrika itafanyika Machi 12, 2024.

Droo hiyo itafanyika Cairo, Misri ambapo droo ya Kombe la Shirikisho Afrika itaanza kuchezeshwa saa nane mchana na ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika itaanza kuchezeshwa saa tisa kamili alasiri.

Timu zilizofuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni Al Ahly (Misri), ASEC Mimosas (Ivory Coast), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Atletico Petroleos (Angola), TP Mazembe (DR Congo), Simba SC (Tanzania), Esperance Sportive de Tunis (Tunisia) na Yanga (Tanzania).

Timu zilizofuzu hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika ni USM Alger (Algeria), Zamalek (Misri), Dreams FC (Ghana), RS Berkane (Morocco), Modern Future (Misri), Abu Salem (Libya), Rivers United (Nigeria) na Stade Malien (Mali).