Dola 100,000 zatolewa kudhamini CECAFA Samia Women Cup

SOKA WANAWAKE

0
1821

Rais Samia Suluhu Hassan atoa dola laki moja za marekani kudhamini mashindano ya CECAFA ya klabu kwa Wanawake yaliyopewa jina la CECAFA Samia Women Cup yanayofanyika nchini Kenya

Katika udhamini huo bingwa wa mashindano hayo atapata kiasi cha dola elfu thelathini, mshindi wa pili kupokea dola elfu ishirini huku mshindi wa tatu kuibuka na kitita cha dola elfu 10

Fedha hizo pia zitatumika katika kutoa zawadi kwa washindi mmoja mmoja na kununulia Tuzo mbalimbali zitakazotolewa katika mashindano hayo