Dodoma Jiji yamtimua kocha Mbwana Makata

0
1930

Klabu ya Dodoma jiji imesitisha mkataba wake na kocha mkuu wa timu hiyo Mbwana Makata kuanzia leo tarehe 23 Februari, 2022.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesema, makubaliano hayo yamefikiwa kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo ya timu katika mashindano mbalimbali ya msimu huu 2021/2022.

Aidha Klabu imetoa shukrani kwa kocha Mbwana Makata kwa mchango wake kwenye timu hiyo.

Dodoma Jiji hawajapata matokeo mazuri hivi karibuni, wametoka kufungwa watoza ushuru kutoka Kinondoni KMC.