Dodoma Jiji imepata ushindi wa kwanza Ligi Kuu ya NBC mwaka huu baada ya kufunga Geita Gold FC goli 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Liti mkoani Singida.
Kwa ushindi huo Dodoma imepanda hadi nafasi ya 9 baada ya kufikisha alama tano.
Timu zote zimeshuka dimbani mara tano ambapo Dodoma imeshinda mchezo mmoja, ikatoka sare miwili na kupoteza miwili, huku Geita ikitoka sare michezo mitatu na kupoteza miwili.