Diamond Platnumz kuburudisha Simba Day, viingilio vyatajwa

0
289

Afisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, amesema Simba itacheza na timu kutoka Burundi ya Vital’O katika kilele cha wiki ya klabu hiyo ijulikanayo kwa ‘Simba Day’ siku ya Jumamosi Agosti 22, katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Manara amesema walipanga kucheza na Al Ahly ya Misri lakini changamoto ya corona imefanya jambo hilo kuwa gumu.

“Tunaamini Vital’O itatupa changamoto nzuri kwenye mchezo huo,” amesema.

Ameongeza kuwa siku hiyo, Simba Day, burudani itatolewa na Twanga Pepeta, Tunda Man, Meja Kunta, Mwasiti na Diamond Platinumz.

Viingilio kwenye sherehe na tafrija hiyo kenye Uwanja wa Uhuru itakuwa Sh. 2,000 na Uwanja wa Mkapa Mzunguko itakuwa 7,000/- VIP C 20,000/-, VIP B 30,000/-, VIP A 40,000/- na kutakuwa na tiketi maalum za Platinum 150,000/