Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ameipongeza Yanga kufuatia ushindi wa goli moja kwa sifuri ilioupata dhidi ya Simba katika mchezo wa watani wa jadi.
Dewji kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika “Hongereni Sana wana Yanga. Mungu akitujalia tutakutana kwenye FA [Kombe la Shirikisho].”
Katika mchezo huo Yanga ilipata bao la ushindi dakika ya 44 kufuatia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Bernard Morrison baada ya kufanyiwa madhambi na Jonas Mkude.