De Gea kusaini mkataba mpya na Man United

0
469

Kipa wa klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza,- David De Gea anatarajia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.

Kulingana na mkataba huo mpya, De Gea mwenye umri wa miaka 27 na raia wa Hispania atakua akipokea mshahara wa Pauni Laki Tatu na Nusu kwa wiki.

United walimnunua De Gea kutoka Atletico Madrid mwaka 2011 kwa ada ya Pauni milioni 19 na amekua mhimili mkubwa kwa klabu hiyo na mchezaji pekee ambaye kiwango chake hakijawahi kushuka.

Uongozi wa klabu hiyo ya Manchester United umesema kuwa De Gea ni bora tofauti na makipa ambao walitangulia ambao walikua na ulinzi imara huku matokeo yao si ya kuridhisha, wakati De Gea ana ulinzi dhaifu na matokeo mazuri.