Dau la Rais Samia la milioni 5 kila goli ni endelevu

0
255

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ameeleza kuwa ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kununua kila goli la Simba SC na Yanga SC litakalofungwa kwenye mashindano ya Afrika inaendelea hadi mwisho wa mashindano.

Amesema katika kila mchezo ambao timu hizo zinazoiwakilisha Taifa zitacheza, kila goli watakalofunga kila timu itapewa TZS miloni 5.

Mwishoni mwa wiki Yanga SC iliondoka na TZS milioni 15 baada ya kuiadhibu TP Mazembe kwa magoli 3-1, huku Simba SC ikitoka mikono mitupu baada ya kupokea kipigo cha magoli 3-0 kutoka kwa Raja CA ya Morocco.